Joslin aeleza sababu ya 'bifu' yake na Mr Blue
Rapa na muimbaji wa muziki wa bongo fleva Joslin ambaye aliwahi kutamba
na ngoma kibao kali amefunguka na kusema yeye na rapa Mr Blue
walizidiana uwezo kimuziki
Joslin akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa
Radio, amesema hajawahi kuwa na bifu na Mr Blue ila anachojua yeye ni
kwamba walizidiana uwezo kwenye muziki kiasi cha wadau, mashabiki kuanza
kuwafananisha.
"Mimi sijawahi kuwa na tofauti na Mr Blue na wala hatukuwahi kuwa na
bifu yoyote ile sema najua mimi na Blue tulizidiana uwezo hivyo kulikuwa
na mchezo wa uwezo tu kati yangu na yeye, sema wadau na mashabiki ndiyo
walianza kutufananisha na kutupambanisha kwa sababu walikuwa wanaona
kama tuna flow na midondoko inayofanana hivi" alisema Joslin
Mbali na hilo Joslin anasema wakati bado hajatoka kimuziki alikuwa
akikutana na Mr Blue na kwamba Blue alishawahi kumtabiria kufanya vizuri
pindi atakapotoka kimuziki kutokana na uwezo wake.
"Kabla sijatoka kimuziki nilikuwa nakutana sana na Mr Blue na alishawahi
niambia, niga siku ukija kutoka wewe watu watapagawa sana" alisema
Joslin
Post a Comment