Ben Pol adai mapokezi ya wimbo ‘Phone’ yamemfanya ajipange upya kwenye video ya wimbo huo
Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol amesema mapokezi mazuri ya wimbo
‘Phone’ aliomshirikisha Mr. EAZI yamemfanya awekeze nguvu nyingi kwenye
video ya wimbo huo.
Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo umekuwa mkubwa kwa muda mfupi tofauti na alivyotarajia.
“Kusema kweli namshukuru Mungu wimbo umekuwa mkubwa sana tofauti na
nilivyotarajia, hata uwekezaji wa video nimelazimika kuwekeza zaidi kwa
sababu nimegundua watu wanatarajia mambo makubwa. Kwa hiyo mashabiki
wakae mkao wa kula kuna mazuri yanakuja kutoka kwenye video yake,”
alisema Ben Pol.
Aliongeza, “Video naweza kusema ni kama tayari nusu, kwa sababu parts za
Mr EAZI akiwa na mimi tayari pamoja na parts zake. Kilichobakia ni mimi
kushoot sehemu zangu pamoja na story ya video na Mungu akisaidia
ikakamilika mapema basi itatoka,”
Muimbaji huyo ni mmoka kati ya wasanii ambao ni zao la THT ambaye bado anafanya vizuri katika muziki.
Post a Comment