DAR ES SALAAM: STAA wa filamu ‘grade one’ na Miss Tanzania 2006, Wema
Isaac Sepetu ameweka rekodi ya ajabu ya kuwa staa wa kwanza nchini
kutumia magari mengi ya kifahari ndani ya kipindi cha miaka kumi
mfululizo, Ijumaa linakuchambulia.
Katika chimbachimba iliofanywa na Ijumaa imebaini kuwa, mlimbwende huyo
mwenye mvuto katika vyombo vya habari hadi sasa ameshateketeza mamilioni
ya shilingi kwa kutembelea magari yenye thamani kubwa, huku kwa sasa
ikidaiwa hana usafiri wa kueleweka.
Toyota Lexus (mil. 40)
Mwaka 2012 aliuanza vema baada ya kudaiwa kununuliwa gari hilo na kigogo
mmoja (jina linahifadhiwa) lenye thamani ya shilingi milioni 35 (sokoni
milioni 28 hadi 35).
Hata hivyo gari hilo hakukaa nalo sana kwani baada ya kupata lingine (Toyota Mark X) aliamua kumpatia mama yake kama zawadi.
Toyota Mark X (mil.35)
Baada ya kuachana na Lexus, alivuta gari jipya (Mark X) ambalo alidai
lilikuwa na thamani ya shilingi milioni 38 (kwa sasa sokoni ni milioni
28 hadi 35).
Katika gari hilo, Wema alidai ameamua kufikia uamuzi wa kulinunua ili kubadilisha mazingira.
Audi Q7 (mil. 80)
Alianza kuonekana nalo kwa mara ya kwanza mwaka 2013 katika Fukwe za
Coco jijini Dar ambapo aliweka picha mtandaoni na kusema kuwa amepata
‘baby’ mpya ambaye yupo naye beach.
Hata hivyo ilikuja kujulikana baadaye kuwa gari hilo alipewa na kigogo
mmoja aliyekuwa akitoka naye kimapenzi kipindi hicho (jina
linahifadhiwa) ambalo alimnunulia kwa bei ya shilingi milioni 80.
BMW 545i (mil. 45)
Alizawadiwa mwaka 2014 na meneja wake, Martin Kadinda katika sherehe ya
siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika alikopanga zamani, Kijitonyama jijini
Dar.
Gari hii lilikuja kuleta mkwaruzano baada ya aliyekuwa bwana’ke, Diamond
Platnumz kukataa kuwa Kadinda hawezi kulinunua. Thamani yake ilitajwa
kuwa ni milioni 56 wakati sokoni linapatikana kwa milioni 40 hadi 45.
Nissan Murano (mil.36)
Siku hiyohiyo pia, aliyekuwa mpenzi wake enzi hizo, Diamond alimkabidhi
Wema gari hilo lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 36.
Diamond ambaye alikuwa akitamba na Wimbo wa Number One alitumia kurasa
zake za mitandao ya kijamii kumpongeza siku yake ya kuzaliwa na kuweka
wazi kuwa ameamua kumzawadia gari.
Range Rover Evogue (mil.140)
Ilikuwa mwaka 2015 katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa
iliyofanyika Millenium Towers, Kijitonyama jijini Dar. Katika usiku huo
aliosindikizwa na mastaa kibao wa filamu Bongo, Wema aliwatoa hadi nje
ya ukumbi huo na kuwaonesha gari hilo ambalo alidai amejizawadia
(pichani juu).
GAZETI LA IJUMAA
Baada ya kuwaonyesha, alitupa madongo kwa Diamond ambaye alikuwa
ameshaachana naye na kusema kuwa si wa kuhongwa vigari vya dola elfu 30
(milioni 30).
Hata hivyo, alidai gari hilo lina thamani ya shilingi milioni 200 wakati sokoni linapatikana kwa bei ya shilingi milioni 140.
Atumia milioni 376
Wakati kukiwa na madai kuwa nyota huyo asiyechuja hivi sasa hana ndinga,
mahesabu yanaonyesha kuwa ukiondoa gari alilozawadiwa kama mshindi wa
Shindano la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ametumia zaidi ya shilingi
milioni 376 kwa ajili ya magari peke yake, rekodi ambayo inaweza kuwa
haijawekwa na staa mwingine yeyote Bongo.
Ijumaa lilimtafuta Wema ili kujua kwa sasa anatumia gari gani lakini
jitihada hazikuweza kuzaa matunda baada ya simu yake kutopatikana.
Paparazi wetu pia alijaribu kufika nyumbani kwa Wema, maeneo ya Ununio
nje kidogo ya Jiji la Dar na kuambiwa kuwa, hayupo lakini ndani kulikuwa
na gari ya silva ambayo haikujulikana ni aina gani na kama ni yake au
ya ndugu yake.
Jitihada za kujua kwa sasa staa huyo mkubwa anatumia usafiri gani zinaendelea.
Post a Comment