0
Wapiganaji wa kundi la al-Shabab

Wapiganaji wa kundi la al-Shabab
Msemaji wa Jeshi la Kenya Luteni kanali Paul Njuguna ameambia BBC kwamba washambuliaji wa kundi la al-Shabab wameshindwa kuiteka kambi ya wanajeshi wa Kenya kusini mwa Somalia ,na kuwa shambulio hilo limetibuliwa na wanagmbao hao kutoroka.
Ameongezea kuwa washambuliaji walitumia magari yaliojazwa vilipuzi lakini hawakufaulu katika shambulio lao.
Al-Shabab wanasema kuwa waliiteka kambi hiyo ya kijeshi katika shambulio la mapema lililoua idadi kubwa ya wanajeshi.
Luteni Kanali Njuguna amekana madai hayo akisema kwamba wanajeshi wa Kenya kwa sasa wanatekeleza operesheni ya kuondoa hasira kufuatia shambulio hilo.
Januari mwaka uliopita, wapiganaji wa al-Shabab walishambulia kambi ya majeshi ya Kenya el-Adde na kuua wanajeshi wengi.
Al-Shabab walisema waliua zaidi ya wanajeshi 100. Jeshi la Kenya halijatangaza idadi kamili ya wanajeshi waliouawa hadi wa leo.

Post a Comment

 
Top