Waziri wa nchi ofisi ya Rais – TAMISEMI George Simbachawene amewataka
wakuu wote wa mikoa kuhakikisha wanawaondoa ombaomba walioko mitaani
pamoja na kuwachukulia hatua watu wazima wanaowatumia watoto katika
shughuli za kuomba.
Waziri Simbachawene amebainisha hayo jijini dar es salaam mara baada ya
kuzindua kitabu kiongozi cha Taifa cha utekelezaji wa sera za huduma kwa
watoto walio katika mazingira hatarishi kwenye mamlaka za serikali za
mitaa ambapo amesema watendaji kuanzia ngazi ya mtaa wahakikishe
wanawakusanya watoto wote walioko mtaani na kutafuta chanzo cha wao
kuingia mitaani na kuwarudisha walikotoka huku wazazi na walezi wao
wakichukuliwa hatua kali.
Katika hatua nyingine waziri Simbachawene amekutana na kufanya
mazungumzo na shirika la misaada la Marekani – USAID ambapo pamoja na
mambo mengine Tanzania imeweka wazi kushindwa kufikia malengo yake
katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Amesema fedha zinazotolewa na wafadhili ni nyingi lakini amekiri kuwa
kuna udhaifu ambao umejitokeza katika matumizi ya pesa hizo ambao
umechangia katika kufikia malengo yanayotarajiwa.
Post a Comment