MAHAKAMA ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, imemhukumu kutumikia
kifungo cha miezi sita jela, Mbunge wa Jimbo la Kilombero kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Lijualikali (30) kwa kosa
la kufanya fujo na kusababisha taharuki.
Hata hivyo, Mbunge wa Mikumi Joseph 'Profesa Jay' Haule (Chadema),
alisema aliwasiliana na viongozi wa kitaifa na Mwanasheria Mkuu wa chama
hicho, Tundu Lissu na kwamba wanakusudia kukata rufaa kupinga maamuzi
hayo.
Profesa Jay ambaye jimbo lake ni jirani na Kilombero linaloongozwa na Lijualikali, alisema hukumu hiyo imemshtua.
Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Timothy Lyon alisema amemhuku kifungo
Lijuakali baada ya kumtia hatiani kwa kosa yeye na dereva wake, kwa kuwa
Mbunge huyo amepatikana na hatia katika kesi tatu huko nyuma na
kuhukumiwa kulipa faini.
Alisema Mbunge huyo anastahili kutumikia adhabu hiyo ya kwenda jela miezi sita.
Post a Comment