0
Arusha. Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama pamoja na Tume ya Kuratibu na Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini wamefanikiwa kukamata magunia 58  dawa za kulevya aina ya bangi na kuteketeza hekari 31 wilayani Arumeru.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari leo amesema operesheni hiyo ilifanyika kwa siku mbili kati ya Januari 10 na 12 mwaka huu katika Kijiji cha Kisimiri Juu Kata ya Uwiro na  walipata magunia 31 pamoja na mbegu Kilogramu 210 ambazo ziliteketezwa kwa moto.

Alisema katika msako huo uliofanyika Kijiji cha Kisimiri Juu pia walifanikiwa kuteketeza jumla ya hekari 19 zilizokua zimelimwa bangi ndani ya mazao mengine.

Kamanda Mkumbo aliongeza kusema kuwa katika Kijiji cha Engalaon Kata ya Mwandeti Tarafa ya Mkulati walikamata magunia 27 ya bangi na kuteketeza hekari 12 za zao hilo ambazo zilikua mbioni kuvunwa .

Post a Comment

 
Top