Hali ya wasiwasi ilikuwa imetanda mahakamani hii leo, wakati jamaa na
marafiki wa raia wa sudan kusini walipowasilisha mahangaiko yao ya
kutoweka kwa raia wawili wa sudan Kusini.
Wakili na mwanaharakati Dong Samuel Luak na mwanachama wa upinzani
Aggrey Esbon Idri, walitoweka siku nne zilizopita. Wakili wa familia ya
raia hao aliwasilisha madai kwamba huenda raia hao wawili wameshikiliwa
chini ya ulinzi mahali ambapo hapajulikani, madai ambayo polisi na idara
ya uhamiaji, wamekanusha na kusema kwamba hawana habari yoyote kuhusu
kupotea kwa raia hao
Jaji wa mahakama kuu ametoa amri kwamba Idara ya uhamiaji kwamba
isiwafukuze nchini raia hao kinyume na sheria na kampuni ya mawasiliano
ya simu za mkononi Safaricom itoe ripoti kamili ya mawasiliano ya mwisho
ya raia hawa.
Akizungumza na BBC, Rebeca Garang, mke wa marehemu John Garang, amesema
kwamba anashangazwa na jinsi mambo yanavyoendelea Juba. Amelazimika
kuhamisha mwanawe kutoka Kenya akiwa na hofu kwamba pia analengwa, hii
ni baada ya kupatina kwa taarifa kwamba mwanawe ni mmoja wa watu kumi na
sita walioorodheshwa na serikali ya Juba kwamba wahamishwe kutoka kenya
hadi sudan kusini
shirika la kupigania haki za kibindamu Human Rights Watch, limesema
kwamba kwa miaka ya hivi karibuni, Kenya imewafukuza viongozi kadhaa wa
upinzani licha ya wao kuorodheswa kama wakimbizi chini ya sheria ya
Kenya
Post a Comment