Mamia ya wananchi Kigoma waandamana na kufunga Zahanati ya kijiji
Katika hali isiyo ya kawaida mamia ya wananchi wa kijiji cha Mwakizega
tarafa ya Ilagala wilayani Uvinza mkoani Kigoma wameandamana na kufunga
siku nzima Zahanati ya kijiji kupinga uhamisho wa muuguzi pekee
katika zahanati ya kijiji kutokana na jinsi anavyowahudumia wagonjwa
vizuri.
Wameeleza kuwa wamechukua maamuzi hayo ili kueleza hisia zao kutokana na
muuguzi huyo Zainab Hassan kupewa uhamisho kwenda zahanati ya kijiji
cha Sunuka, hali ambayo itaathiri upatikanaji wa huduma za afya huku
kaimu afisa mtendaji kata ya Mwakizega Mariam Ulimwengu akieleza kuwa
huduma zilisimama baada ya kufungwa kwa kituo na wananchi licha ya
kwamba kuna watumishi wengie wawili.
Kutokana na hali hiyo mbunge wa jimbo la Kigoma kusini Husna Mwilima na
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza Jackson Mateso
wamelazima kutumia hekima kubatilisha maamuzi hayo na kuonya watumishi
wanaonyanyasa wagonjwa.
Post a Comment