Msanii wa bongo flava ambaye ndiyo anaanza kuchipukia, Harmo Rapa,
amesema kuwa hana mpango na wala hawezi kubadili jina hilo lililompa
umaarufu kwenye muziki kwa hofu ya kupoteza mashabiki wake.
Harmo Rapa
Msanii huyo anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la 'USIGAWE
PASI'. ametoa msimamo huo kupitia eNewz ya EATV iliyomtafuta kuzungumza
naye kuhusu mpango wa kubadili jina lake na kutotumia jina la 'Harmo
Rapa'.
“Mimi sina mpango wa kubadili jina langu kwa sababu naogopa kupoteza
mashabiki zangu na ukiangalia kwa sasa jina la Harmo Rapa limeshakuwa
kubwa na tayari nimeshajitengenezea mashabiki kupitia jina hilo”
Pia amesema kuwa hana mpango wa kwenda WCB na wala hahitaji msaada
wowote kutoka kwao huku akionesha jeuri kuwa angeweza kutoka hata bila
kutumia jina hilo. "Hata bila kufananishwa na Harmonize mimi ningetoka
tu"
Harmo Rapa ni moja kati ya wasanii ambao wamepata kiki ya kutosha
kutokana tu na muonekano wake ambapo watu wengi wamekuwa wakimfananisha
na Harmonize kutoka WCB.
Msanii huyo hivi karibuni katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa
Radio alijifananisha na Fid Q na kuwaacha watu midomo wazi.
Post a Comment