Pesa Kupotea Mitaani… Machangu Watoa Kilio Chao kwa JPM
Dar
es salaam: Kufuatia hali ngumu ya kimaisha kutokana na pesa
kutopatikana kirahisi kama ilivyokuwa awali, akinadada wanaofanya
biashara haramu ya kuuza miili yao ‘machangudoa’ katika Jiji la Dar
wametoa kilio chao kwa Rais John Magufuli ‘kulegeza’ kidogo kwani
wanakufa njaa.
Machangu hao waliamua kufunguka hivyo hivi karibuni baada ya kuhojiwa na
mapaparazi wa OFM waliokuwa wakifanya uchunguzi kuhusiana na biashara
hiyo katika kipindi hiki ambacho kila mtu analia akisema ‘pesa imekauka
mifukoni’.
Hali ikoje?
Katika utafiti huo uliofanyika katika maeneo ya Sinza Afrikasana,
Kinondoni Makaburini na Buguruni jijini Dar, biashara hiyo imeonekana
kudoda huku wengi wakieleza kuwa, hali hiyo imetokana na ugumu wa
maisha.
Akizungumza na paparazi wetu, dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la
Pili, Mkazi wa Buguruni jijini Dar anayefanya biashara hiyo maeneo ya
Sinza Mapambano alisema:
“Kiukweli hali ni mbaya sana, unajua wateja wetu wengi walikuwa wale
ambao walikuwa wakipata pesa za kimagumushi, sasa baada ya Magufuli
kubana, watu wamekuwa makini sana na pesa zao.
“Matokeo yake sasa, wateja wamekauka, unaweza kuja kijiweni, ukapigwa na
baridi wee bila kupata mwanaume, ukarudi nyumbani mikono mitupu, kwa
kweli hali ni mbaya.”
Machangudoa wakijiuza usiku.
Naye Betty anayejiuza maeneo ya Sinza Mori jijini Dar alisema; “Kwa
kweli itafika wakati inabidi tukalime, nimefanya biashara hii kwa muda
mrefu lakini sijawahi kukumbana na ukata kama huu.
“Kuna miezi ambayo tunajua watu hawana pesa lakini kuna ile ambayo
tunajua biashara itakuwa poa ila sasa hivi wateja hakuna mwanzo mwisho,
yaani Magufuli ni noma, angelegeza kidogo.”
Hata hivyo asilimia kubwa ya machangu waliozungumza na OFM na kuulizwa
kwa nini wang’ang’anie biashara hiyo hatarishi walisema, eti ndiyo
ambayo imekuwa ikiwasaidia katika kuendesha maisha yao kwa muda mrefu.
“Wewe unadhani mimi nitakwenda kufanya nini, sijasoma wala sina ujuzi
wowote, nimefanya biashara hii kwa muda mrefu, nimeichukulia kama ajira
kwangu, sasa hali ikiwa mbaya hivi nikalie wapi? Watoto nitawasomesha na
nini? Pango nitalipa na nini?” alisema dada mmoja aliyegoma kutaja jina
lake.
Biashara kwa promosheni sasa
Katika maeneo ambayo OFM walitembelea, wasichana hao wakiwa wamevalia
nguo za kihasara walionekana kugombea kila mteja aliyekatiza mbele yao
na wakati mwingine kufikia hatua ya kupigana.
Aidha, tofauti na kipindi cha nyuma ambacho ukikutana na dadapoa anakupa
bei ya kwenda kulala naye na ya ‘short time’, sasa hivi ni kwa
promosheni na unaulizwa una shilingi ngapi, kiasi utakachotaja ni ngumu
kukataliwa.
Wamepagawa
Kufuatia ukata huo, wadada wengi wanaofanya biashara hiyo wanaonekana
kudata, ambapo wengi wamekuwa wakivuta bangi na kulewa sana kiasi kwamba
ukikutana naye uso kwa uso, utaona dhahiri ni mtu aliyekata tamaa.
Wizi umeongezeka
Uchunguzi wetu umebaini kuwa, kutokana na wateja kupungua baadhi ya
dadapoa hao wameanzisha tabia ya kuwaibia watu simu na pesa hasa katika
maeneo ya Kinondoni na Buguruni.
Post a Comment