Mesut Ozil yuko tayari kusaini mkataba mpya na Arsenal lakini anataka
kujua kama meneja Arsene Wenger atabaki kwenye klabu hiyo baada ya
mwisho wa msimu huu.
Ozil (kushoto) na Wenger kwenye mazoezi
Mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni wa msimu huu wakati mikataba ya
Ozil na mchezaji mwenzake Sanchez inamalizika baada ya miezi 18.
Ozil amesema kuwa anafurahi sana kubaki kwenye klabu ya Arsenal na
amewaambia viongozi wa timu hiyo kuwa angependa kuongeza muda wa mkataba
wake.
"Nina furaha sana ndani ya Arsenal na nimeiacha klabu itambue hilo
kwamba nipo tayari kusaini mkataba mpya."Alisema Ozil akiongea na
waandishi wa habari za michezo za Ujerumani.
"Mashabiki wanataka nibaki na sasa ni uamuzi wa klabu.
"Wanajua kwamba nipo hapa kwa sababu ya Arsene Wenger. Yeye ndiye
aliyenileta na yeye ndiye anayeamini nilichonacho. Klabu pia inajua
kwamba nataka kuwa muwazi na kile meneja anataka kufanya."
Post a Comment