0
Kipara ni mtindo unaotumiwa na warembo wachache duniani. Warembo kama Amber Rose na zamani Kajala, walikuwa wakitambulika haraka kwa style hiyo.

Kuna wakati pia Shaa alikuwa mpenzi wa kipara lakini miaka ya karibuni akawa akipigilia weaving na rasta za kila aina kama warembo wengine. Ni labda katika kutaka kuwa na Valentine’s Day ya tofauti mwaka huu, Shaa ameamua kukirudisha kipara chake. Good news ni kuwa, bae – Master J, amependa.

Kitu kizuri kuhusu kipara kwa wanawake, ni kuwa bajeti ya nywele za weaving inapungua. “About last night…Baby kafurahia kipara..budget imenyooka! #REDHOTVALENTINE,” Shaa ameandika kwenye picha aliyoweka Instagram.

Post a Comment

 
Top