0
WALIMU 98 wa shule za msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai wanatarajiwa kustaafu kwa mpigo utumishi wa umma mwaka huu.

Idadi hiyo ya walimu wanaostaafu inaufanya mkoa wa Kilimanjaro sasa kuwa na upungufu wa walimu 2,398 wa shule za msingi.

Akizungumza mjini hapa mwishoni mwa wiki kuhusu upungufu huo katika mkutano wa baraza la wafanyakazi, Kaimu Ofisa Utumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Habiba Mtunguja, alisema takwimu hiyo inawagusa zaidi walimu wa shule za msingi.

“Kwa mwaka huu peke yake, kumbukumbu zetu zinaonyesha kwamba kuna watumishi wenzetu 98

wanatarajiwa kustaafu na wengi wao ni walimu wa shule za msingi, sasa mnapata picha halisi ilivyo wakati huu ambao tunafikiria kujiimarisha hasa sekta ya elimu,” alisema Mtunguja.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Yohana Sintoo akizungumza katika mkutano huo alimtaka Ofisa Utumishi huyo kuyafanyia uchunguzi mambo ambayo bado ni changamoto na kuyatafutia ufumbuzi kabla hayajaibua malalamiko, hasa katika sekta ya elimu.

Mwishoni mwa mwaka jana, Ofisa Elimu wa mkoa huo, Euprasia Buchuma, alinukuliwa na Nipashe akisema hali ni mbaya zaidi katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ambayo walimu zaidi ya 400 wanatarajia kustaafu utumishi wa umma mwaka huu.

Wakati hali hiyo ikijitokeza, inaelezwa kuwa serikali inatarajiwa kuajiri walimu wapya 35,411 wa shule za msingi na sekondari nchini ili kuongeza idadi ya walimu.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top